Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentinia, Lionel Messi amesaini mkataba mpya utakaomuweka ndani ya timu hiyo hadi mwaka 2020/21.

Mkataba huo utamuweka staa huyo wa Argentinian hadi msimu wa mwaka 2020/21 huku kipengele cha ununuzi kikiwa ni euro milioni 700 ili kuepusha yale yaliyojitokeza kwa Neymar wakati alipohitaji kusajiliwa na PSG.

Kwa usajili huo utamfanya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, kuwa ndani ya klabu hiyo kwa miaka 17.

Lionel Messi amejiunga na Barca mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 13 alipo wasili akitokea klabu ya Newell’s Old Boys nchini Argentinian.

Baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu na kuvutia katika timu mbalimbali za vijana ndipo akaitumikia timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 ukiwa mchezo dhidi ya FC Porto kisha kuanza rasmi kucheza akiwa na umri wa miaka 17 dhidi ya Espanyol.

Leo Messi amekuwa ni mchezaji ambaye anavunja rekodi zilizowahi kuwekwa kilasiku hadi kuwa moja kati ya mchezaji bora katika historia ya soka, kwa kuwa na idadi mengi ya mabao, mataji, rekodi akiwa yeye kama yeye na hata tuzo mbalimbali akiwa na timu yake ya Barcelona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *