Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi ameisadia timu yake kushiriki kombe la dunia baada ya kufunga mabao matatu kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Ecuador.

Luis Suarez alifunga mabao mawili na kuwawezesha Uruguay kulaza Bolivia 4-2 na kufuzu mashindano hayo.

Colombia pia wamesonga mbele baada ya kutoka sare 1-1 ugenini Peru na kuwa timu ya nne kufuzu mashindano hayo.

Peru walimaliza wa tano katika michuano ya kufuzu Amerika Kusini na sasa watakutana na New Zealand katika mechi mbili za muondoano za kufuzu.

Lakini nyota wa Arsenal Alexis Sanchez na taifa lake la Chile wako nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa 3-0 ugenini Brazil.

Argentina walianza siku wakiwa nambari sita na kwenye hatari ya kutofuzu kwa mara ya kwanza tangu 1970.

Aidha, walianza vibaya katika mechi hiyo iliyochezewa mji ulio nyanda za juu wa Quito. Wenyeji walijiweka kifua mbele baada ya sekunde 38 kupitia bao la Romario Ibarra, bao la kasi zaidi ambalo Argentina wamewahi kufungwa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia.

Alisawazisha baada ya dakika 12 aliposhirikiana vyema na nyota wa zamani wa Manchester United Angel di Maria.

Bao lake la pili alilipata dakika nane baadaye na kisha akafunga la tatu na la ushindi kipindi cha pili.

Hata hivyo, Brazil walishambulia na Jesus alipata lango likiwa wazi baada ya mchezaji mwenzake wa Manchester City Claudio Bravo kukwama uwanjani na hivyo safari ya Chile kwenda Kombe la Dunia ikafikia tamati hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *