Mtayarishaji wa muziki wa Bongo fleva nchini, Mesen Selekta kutoka De Fatality studios amesema kuwa yeye ndiye producer pekee anayetengeneza muziki halisi wa Singeli hapa nchini tofauti na watayarishaji wengine.
Mesen amefunguka kwa kusema maproducer wengi wanajaribu kutengeneza Singeli lakini wanakosea kwa kufananisha muziki huo na mnanda ambapo ni vitu viwili tofauti lakini kwa upande wake anajua kutofautisha.
Mesen ameongeza kwa kusema kuwa kuna muziki unaitwa Singeli, kuna mnanda na ladha, muda mwingine baadhi ya producer wanajaribu kutengeneza Singeli lakini inakuwa sio Singeli kutokana wanachanganya ladha ya mnanda.
Mesen ametayarisha hits nyingi za Singeli zikiwemo ‘Hainaga Ushemeji ya Man Fongo, ‘Sembe Tembele’ ya Sholo Mwamba na wimbo mpya wa Profesa Jay, Kazi aliomshirikisha Sholo Mwamba.
Producer huyo kwasasa anafanya vizuri kwenye muziki wa Singeli ambao umeonekana kushika kasi hapa jijini Dar es Salaam kutokana na kuzoa mashabiki wengi kutoka maeneo ya uswahilini.
Muziki wa Singeli ulikuwa unaonakana kama muziki wa kihuni lakini kwasasa umebadilika na kuwa dhahabu mpaka kupelekea wadau kuanza kuwekeza kwenye muziki huo.