Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Saraphina ameonekana kufanya vizuri kwenye muziki wa Bongo fleva toka alivyoingia kwenye muziki.

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Meneja wa msanii huyo ameandika

“Ni safari iliyoanza mwezi wa pili mwaka Jana, ambapo rasmi tulianza kutoa kazi za @saraphina__tz haijawa safari nyepesi ni ngumu yenye mabonde na milima ya kutosha ila iliyoleta funzo, furaha , matumaini na malengo mapya na makubwa.

Saraphina__tz na timu hatukuchoka tulitoa wimbo baada ya wimbo na kuendelea kuwapa watanzania burudani waliyostahili.

Kama wahenga walivyosema atafutaye hachoki ama kwa hakika hatukuchoka na matunda tunayaona Sasa. Haya yametokea wakati @saraphina__tz akiwa msanii ambaye hayupo kwenye lebo yoyote KUBWA na soon MELANIN QUEEN anaenda kutambulisha MUSIC LABEL yake.

UPONYONYO ni wimbo ulitengeneza historia mpya kwenye safari ya Muziki ya @saraphina__tz na mapokezi makubwa watanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla imempa wazungu walisema NUMBERS DO NOT LIE kwa sisi wabantu NAMBA HAZIONGOPI.

UPONYONYO umefanya vizuri kwenye audio platforms nyingi na kwa Boomplay umefanikiwa kufikiksha streams milioni moja (1M) ndani ya muda mfupi pamoja na kumfanya #Saraphina kuwa katika chati ya wanamuziki wanaofutiliwa Zaidi

Pia ameendelea kuandika ndio usiseme ndio wimbo wenye namba kubwa kwa Sasa kwa challenges mbili tofauti UPONYONYO Ina milioni tisa (9M) na #NIPONYONYO Ina milioni tatu na laki name(3.8M) YouTube imefikisha ONE MILLION VIEWS (1,000,000,).

Asanteni watanzania tuendelee kuburudika na #UPONYONYO kwenye Platform zote za dijitali WIMBO NI WENU #UPONYONYO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *