Baada ya uongozi wa lebo ya Konde Gang kutangaza kuachana na wasanii wake, Killy na Cheed meneja wa wasanii hao afunguka.

Meneja huyo anayeitwa, Lawi Cosmas amesema kuwa ni mapema kusema chochote kwa sasa kwakuwa taarifa hiyo nao wameiona kwenye mitandao na hawajapata barua rasmi ya kimaandishi.

Amesema kuwa “Hata sisi ndugu mwandishi na wasanii wangu hatujui nini kimetokea hadi sasa, naomba unipe muda mpaka tuwasiliane na uongozi tutakuja  na tamko letu  rasmi kuhusu hatua hii.

Meneja huyo amebainisha kuwa katika maamuzi hayo hawajashirikishwa kwani hata juzi katika kundi lao la WhatsApp la ofisini walitakiwa kuhudhuria bila kukosa katika sherehe ya kutimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwa  lebo ya Konde.

Kwa miaka miwili waliyokuwepo Konde Music,Killy aliweza kutoa nyimbo nne ikiwemo Mwisho, Vumilia , Roho na Ni Wewe wimbo aliomshirikisha Harmonize. Kwa upande wake Cheed akiwa konde alitoa nyimbo tatu ikiwemo Wandia, Final na Ndoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *