Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay ajulikanae kama Chambuso amekanusha taarifa kuwa msanii wake huwa anachukua hela alafu atokei kwenye show.

Chambuso amesema hayo baada ya siku za hivi karibuni kuibuka taarifa kuwa mwanamuziki Aslay huwa anachukua hela kwa maprompota wa muziki alafu atokei kwenye show jambo ambalo meneja huyo amekanusha vikali.

Chambusoa amesema kuwa yeye na msanii wake hawajawahi kula hela ya mtu yeyeto bila kufanya show hivyo jambo hilo halina ukweli wowote.

Tetesi hizo zilikuwa zikiendelea mitandaoani kuwa huwa wanachukua hela bila kwenda kufanya show kwa baadhi ya maeneo wanatakiwa kwenda kwenye show hizo.

Chambuso amesema kuwa hadhani kama mtu atakubali hela zake zichukuliwe na tusitokee kwenye show kwasababu wangekuwa tayari washafungwa kama sio kupelekwa polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *