Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameipokea meli ya jeshi la majini kutoka China ambayo imewasili nchini kwa ajili ya kutoa huduma ya bure kwa wagonjwa kuanzia leo hadi Ijumaa Novemba 24 mwaka huu.

Makonda amelipongeza jeshi hilo la China kwa kuiletea Tanzania huduma hiyo bora na ya bure kupitia meli hiyo ambayo ni pili kwa ukubwa duniani.

 Pia Makonda amesema kuwa hayo yote ni matokeo ya ushirikiano baina ya  nchi hizi mbili ulioanza muda mrefu na jeshi hilo ni miongoni mwa taasisi zinazoendelea kuuimarisha.

Makonda amewataka Watanzania kufika kwenye meli hiyo kuanzia leo ili waweze kunufaika na matibabu ya bure.

Makonda ameongeza kwa kusema kuwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa sugu, yenye kuwaletea matatizo kila mara na mengine yanayowasibu wanatakiwa kufika kwa ajili ya matibabu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *