Mwanamuziki wa miomdoko ya Singeli, Meja Kunta amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu kutumia jina lake kutapeli watu kupitia mitandao ya kijamii.

Ni siku kadhaa Msanii huyo toka apishane kauli na uliokuwa uongozi wake,kuna baadhi ya watu wametumia suala hilo kama chanzo cha kuwatapeli watu mitandaoni kwa kutumia picha na jina la lake.

Picha iliyopostiwa na hiyo akaunti fake iliandikiwa maneno yanayosomeka “hivi jamani mimi ni nani mpaka nikiomba msaada mnaanza kunishangaa na kupoteza uaminifu mnajua kabisa niko kwenye matatizo au kisa mimi msanii ndio nisisaidiwe kweli nimeamini tenda wema nenda zako”.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram  amepost picha hiyo na maneno yake na kuandika “Jamani mnao tumia mitandao kwa majina ya watu tunaomba mtumie vizuri ili kusupport kazi za wale mnao tumia majina yao.

Ameendelea kwa kuandika kuwa msitumie kuomba watu pesa na kuchafua kazi au thamani ya mtu sio vizuri mimi sina account Facebook na sijaomba msaada wa aina yeyote ivyo epukeni matapeli.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *