Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na mbunge wa Bunda, Esther Bulaya wamepigwa marufuku kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19.

Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo leo mjini Dodoma kutokana na vitendo vyao vya utovu wa nidhamu.

Kamati ya Maadili imesema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao.

Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *