Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo.

Mdee, alikamatwa na Polisi siku sita zilizopita kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi kwa madai ya kumkashifu Rais John Magufuli.

Hapi aliagiza Mdee akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa 48 kwa makosa hayo pamoja na ya uchochezi.

Mbunge alikamatwa na kupelekwa kituo cha Oysterbay baada ya hapo akahamishwa na kupelewa kituo kikuu cha Polisi (Cetral) jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *