Aliyekuwa mchezaji wa kikapu nchini Marekani, Dennis Rodman amefanya tena ziara nchini Korea Kaskazini.
Nyota huyo wa zamani wa NBA amefanya ziara ya kibinafsi nchini humo kwa ajili ya kukutana na Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un.
Ziara ya staa huyo inakuja siku chache kukiwa na mgogoro kati ya Marekani na nchi Korea Kaskazini kutokana na nchi hiyo kurusha makombora ya kinyuklia.
Rodman aligonga vichwa vya habari baada ya kufanya urafiki na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, wakati wa ziara zake za awali mwaka 2014 na 2014 nchini Korea Kaskazini.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Marekani inasema kuwa inafahamu ziara yake na kusema kuwa “Tunamtakia mema, lakini timetoa onyo mwa raia wa Marekani na kuwashauri wasisafiri kuenda Korea Kaskazini kwa usalama wao,”.
Mgogoro kati ya Marekani na Korea Kaskazini umekuwa mkubwa chini ya utawala wa Rais Donald Trump, ambaye anasema kuwa anahofia mzozo mkubwa huenda ukaibuka kati ya nchi hizo mbili.
Akizungumzaa kwemye uwanja wa ndege, bwana Rodman alisema ” Nina furaha kuwa Trump anafarahia sababu kuwa mimi niko hapa na ninajaribu kutimiza kitu fulani ambacho sisi sote tunahitaji.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chicago Bulls, wakati mmoja alimshauri Rais Barack Obama ampigie simu Bwa Kim, akisisitiza kuwa wote walikuwa mashabiki wa mpira wa kikapu.
Hata hivyo ziara zake zinatajwa na vyombo vya habari nchini Marekani kuwa diplomasia ya mpira wa kikapu.