Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama hicho hakiwezi kutetereka au kufa kwa kiongozi au mwanachama kuhama.

Amesema kuna mkakati mkubwa unaotumia fedha unaofanywa kuwalaghai viongozi na wanachama wake kukihama chama hicho.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa vijana wa chama hicho, Patrobas Katambi kutangaza kujiunga na CCM.

Mbowe amesema kuwa badala ya nguvu na fedha kuzielekeza kujenga viwanda wao nguvu wamezielekeza kushawishi viongozi wetu, wamewashawishi wengi na Katambi ni miongoni ingawa wengine wamekataa.

Mbowe amesema, “Katambi alikuwa katika majukumu ya chama na aliwaaga wenzake anakwenda kumuguza mama yake mgonjwa hivyo akakatiwa tiketi ya ndege, kumbe alikuwa anakwenda kukamilisha dili ambalo naambiwa limetumia saa 48 kukamilika.”

Amesema Chadema ilipofika haiwezi kufa kwani imejijenga na hapo walioondoka lakini mpaka sasa kimeendelea kuwapo.

Mbowe amesema mwitikio wa wananchi katika kampeni za udiwani kwenye kata 43 umeishtua CCM ikiwamo kuhama kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *