Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa ile hofu iliyokuwepo kwa Tundu Lissu sasa imekwisha kwania anaendelea vizuri tofauti na hapo awali.

Mbowe amesema hayo kutokea nchini Kenya alipokwenda kumuuguza Tundu Lissu ambapo amesema kuwa Mbunge huyo sasa anaweza kuzungumza japo anaendelea kupatiwa matibabu na kudai pia ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine.

Pia Mbowe amewataka wananchi kutosikiliza taarifa za watu wengine kuhusu hali ya mgonjwa na kusema taarifa rasmi juu ya hali ya mgonjwa itatolewa na wao ambao wapo na mgonjwa Nairobi Kenya.

Mbali na hilo Freeman Mbowe amedai kuwa Mbunge huyo hana athari zozote zile kwenye kifua chake kama ambavyo baadhi ya taarifa zinasema kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kudai Mwanasheria Mkuu huyo wa CHADEMA yupo imara.

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyopata, ambapo mpaka sasa yuko huko kwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *