Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amesema ameshangazwa kupigwa marufuku kutoa salamu ya vyama vingine katika mikutano ya uchaguzi inayoendelea kufanyika huku akidai sheria hiyo haipo bali ni sheria ya hofu.
Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa yupo katika muendelezo wa kumuombea ridhaa mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia (CHADEMA), Salum Mwalimu kuwa Mbunge wa eneo hilo katika siku zijazo za usoni ambapo kwa sasa zimebakia takribani siku 12 tu uchaguzi mdogo kufanyika.
Pamoja na hayo, Mbowe ameendelea kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema “nikashangaa kidogo, tukija kwenye mkutano hapa Kinondoni hatuji kuzungumza na wanachadema peke yao maana uwanja huu wapo wanawacuf, wanaccm sasa iweje uniambie Mbowe usitoe salamu ya CUF katika mkutano. Hiyo sheria katika uchaguzi haipo ni sheria ya hofu kwa hiyo mimi natambua uwanjani hapa wapo wanacuf na nina haki ya kuwasalimia wote”.
Kwa upande mwingine, Mbowe amesema kusalimia ni hiari yake hivyo hawezi kupangiwa kufanya hivyo.