Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni Profesa wa ajabu ambaye anaweza kubomoa chama alichokijenga mwenyewe.

Mbowe amesema kwamba hana ugomvi wowote na Prof Lipumba ingawa amekiri atakuwa muongo akisema kwamba anamuheshimu kwani anatumika katika kukivuruga chama alichokuwa akikiongoza kwa muda mrefu.

Pia Mbowe amesema kwamba wakati CUF ikishirikiana na UKAWA kwa ujumla kutafuta kura na kuongeza wabunge wa chama hicho bungeni, yeye Prof Lipumba alikuwa mafichoni na anamshanga sasa hivi anavyorudi ndani ya chama hicho na kutaka kukisambaratisha.

Pamoja na hayo Mbowe amedai kwamba Spika wa Bunge pamoja na Msajili wa vyama vya siasa wanatumika katika kuibomoa CUF na kuongeza kwamba hataacha kusema ukweli kwani hakuna mtu yoyote anayemuogopa isipokuwa Mungu pekee.

Ameongeza kwamba kasi inayotumika kuibomoa CUF inatumika pia kuibomoa CHADEMA na kuweka wazi kwamaba siku chama cha Chadema kikiuliwa labda awe amefariki lakini siyo wakati huu ambao bado anapumzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *