Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelaani kitendo cha wabunge 8 wa upinzani kukamatwa na jeshi la polisi kwa madai yakutaka kumpiga mbunge wa CCM Juliana Shonza.

Freeman Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni aliyasema hayo  jana Dodoma baada ya kutoka mahakamani na kudai kuwa wao wanaamini kuwa mahakama itatenda haki kwa wabunge hao.

Pia Mbowe amesema kitendo cha Spika wa Bunge, Job Ndugai kulivalia njuga suala hilo ni jambo ambalo yeye limemsikitisha sana kama kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni.

Mbowe amesema kuwa “Kitendo cha kuwapeleka polisi na kuwashtaki wabunge wetu na Spika wa Bunge kushadadia jambo hili limenisikitisha sana

Katika watuhumiwa wote nane, mtuhumiwa mmoja ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ubungo, Mbunge Saed Kubenea jana  alipandishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa moja la shambulio la kawaida hivyo alidhaminiwa na shauri hilo upelelezi wake bado haujakamilika hivyo kesi itatajwa tena tarehe 26, Julai 2017 Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *