Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameiomba serikali itoe upendeleo kwa shule zote ambazo wazazi wamejitahidi na kuanzisha mabweni kwa ajili ya kidato cha tano na sita ili yaweze kukamilika.

Mbowe ameyasema hayo katika kipindi cha maswali na majibu bungeni ambapo ameiomba serikali isaidie wazazi ambao wameonyesha nia ili shule hizo ziweze kufaidisha wengi hasa katika jimbo lake la Hai.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jaffo amesema kutokana na umuhimu wa elimu na namna ambavyo baadhi ya wazazi wamejitoa ni lazima serikali itafanya linalowezekana kuweza kuwaunga mkono.

Jafo amesema kuwa Serikali itaweka kipaumbele katika eneo hilo na kweli kuna maeneo ambayo tunapaswa kuwapongeza wazazi wote wanaojenga mabweni ili wanafunzi wanaofaulu wasikose sehemu za kusomea na kulala.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *