Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe amedai kuwa anafahamu baadhi ya viongozi wa Chadema wapo hatarini na hata kufikia kuitwa viherere kwa kujiweka mbele kwenye tukio la Lissu
Mbowe amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari akielezea maendeleo ya hali ya Lissu ya kiafya ambaye anatibiwa huko Jijini Nairobi baada ya shambulio la risasi zaidi 30 kwenye gari lake.
Mbowe amesema kuwa kamwe hawatathubutu kurudi nyuma katika suala la kumpigania Lissu wala kukiri umauti na badala yake wataendelea kupambana kwa maombi na mikakati.
Mbowe amesema “Kuna wengine tunaitwa viherehere. Hatutarudi nyuma wa kumuogopa yeyote.Tunajua kuna nini kinapangwa, hatutakiri umauti tutaukataa kwa nguvu zote. Hatuwezi kusema tupo tayari kufa maana ulimi ukikiri umauti ndivyo itakavyokuwa”.
Katika upande mwingine Mbowe amewaahidi wananchi na Watanzania wote kwa ujumla kuwa kuanzia leo zitaonekana picha za Lissu akiwepo hospitalini ili kuthibitisha kauli yake ya kwamba kiongozi huyo ameimarika kiafya.