Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso kutoka WCB ameweka wazi kuwa February 14 ataachia albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la “Definition Of Love”.
Mbosso amesema kuwa albam hiyo imeshakamilika na inatarajia kutoka siku ya sikukuu ya wapenda nao hivyo wamewataka mashabiki wake kuisubilia albam hiyo kwani ina nyimbo nzuri sana.
Pia Mbosso ameeleza namna alivyokata tamaa ya muziki baada ya kundi la Ya Moto Band kusambaratika na kukaa kwa muda mrefu bila kutoa nyimbo.
Kutokana na kukata tamaa za muziki Mbosso amesema kuwa aliamua kujiingiza kwenye mambo ya Mpira na kuwa mchezaji kabisa hadi kuisaidia timu yao kufanya vizuri kwenye mashindano.
Amesema kuwa baada ya kukata tamaa za muziki, siku moja alikuja Rich Mavoko alienda kwao na kumshawishi kujiunga na lebo ya Wasafi ambapo hadi leo yupo kwenye lebo hiyo.