Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso amefunguka kuhusu tatizo la ugonjwa wa moyo ambalo limemwandama tangu akiwa mtoto.

Mbosso amesema kwamba ugonjwa huo unasababishwa na mafuta kuwa mengi kwenye mishipa ya damu ya kwenda kwenye moyo.

Dalili alilozitaja za ugonjwa huo ni pamoja na maumivu upande wa kushoto wa kifua, viungo kupoteza hisia na kwake anatetemeka vidole.

Kwa kitaalam ugonjwa wa mtu kuwa na mafuta mengi kwenye damu huitwa Familial hypercholesterolemia ambao ni ugonjwa wa kurithi.

Ugonjwa huu unamweka mgonjwa katika hatari ya mishipa ya damu kuziba katika umri mdogo na hivyo kusababisha moyo kukosa Oxygen.

Mbosso amesema tangu atambue kuwa ana ugonjwa huo wa moyo amekuwa akimtembelea daktari wake mara kwa mara na kuyafuata maagizo yake katika juhudi za kutaka kupona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *