Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso amrfunguka na kusema kuwa amekuwa akisumbuliwa na Tatizo la Moyo ambalo limekuwa likimtesa siku nyingi japo ni wachache ambao wanafahamu hilo.

Mbosso amesema kuwa tatizo hilo huwa linamsumbua sana japokuwa wachache wanaofahamu kuhusu ugonjwa huo unaomsumbua.

Mbosso amesema “Nina Matatizo makubwa sana ya Moyo yananitia unyonge sana naweza nikalala usiku nashtuka upande wa kushoto unauma sana, Ni maradhi ambayo yananisumbua muda mrefu sana”.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Mimi Mzito sana kuongea vitu vyangu, maradhi yangu yamesababishwa na kuziba mafuta kwenye Mishipa ya Moyo na Wataalam wamesema nisipotibiwa naweza nisizae tena.

Mbosso ametoa ushauri kwa mashabiki wake kuwa inatakiwa wafanya checkup ya miili yao ili kujua wanasumbuliwa na kitu gani ili waweze kutibiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *