Mwanamuziki machachari wa Bongo Fleva, Harmorapa anatarajia kuwa balozi wa kinywaji kiitwacho Swala.
Hamorapa amefunguka kuwa yupo katika mazungumzo na kampuni inayozalisha kinywaji hicho na anatarajia kupata dili nono ya kukitangaza kinywaji hicho.
Mwanamuziki huyo ambaye anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Kiboko ya Mabishoo’ amesema kuwa dili hilo likifanikiwa atajisikia vizuri sana kutokana na ubalozi huo.
Harmorapa amejizolea umaarufu kupitia mitandao ya kijamii kutokana na tabia yake ya kupenda ‘kiki’ kupitia mitandao hiyo.
Hivi juzi Harmorapa alitrend kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutimua mbio alivyoona kitendo cha askari akimtolea bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye