Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, MB Dogg alia na Serikali juu ya watu wanaopiga pesa kupitia kazi zake kwenye platforms mbalimbali.
MB Dogg amefunguka kuwa kuna ukiukwaji wa Sheria za Hakimiliki hali inayosababisha wasanii wengi wakongwe kupitia wakati mgumu kwa kutonufaika na kazi zao.
Msanii huyo ameiiomba Serikali kuingilia kati jambo hilo ili wasanii wakongwe wafaidike na kazi zao za nyuma kwani wamefanya muziki kwa muda mrefu bila mafanikio.
“Sheria za ukiukwaji wa HAKIMILIKI zipo na zifuatwe ili iwe fundisho kwa wadau na wasanii, pia kuwa makini na majina yao kutumika vibaya”.
Mb Dogg alitamba zamani na nyimbo zake kama Latifa aliomshirikisha Madee na kufanya vizuri miaka hiyo ya nyuma.