Kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ akichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa ambaye mkata wake unamalizika mwezi Machi mwaka huu.

Mayanga ataanza majukumu yake kwa kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.

Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).

Shirikisho la Soka nchini TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.

Mayanga kwa sasa ni kocha wa Mtibwa Sugar ambapo amebadilishana na Kocha Mexime ambaye kwa sasa anafundisha kagera Sugar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *