Muigizaji wa Bongo Movie, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amesema kuwa hata kama wenzake watamcheka kwa sababu hajapata mtoto lakini bado ana matumaini ya kupata mtoto.

Muigizaji huyo amesema hayo baada ya baadhi ya watu kuanza kumshambulia muigizaji kwa kukosa mtoto mpaka sasa hivi.

Maya alisema kuwa anajua wasanii wenzake wengi wana watoto na wapo wanaomcheka na kumshangaa lakini sababu hiyo pekee haiwezi kumfanya yeye akakurupuka kumsaka kwa udi na uvumba.

Amesema kuwa “Yaani siwezi kuharakisha kwenye suala la uzazi kabisa, hata nikizaa na miaka hamsini haina shida ili mradi tu nizae na baba mwenye kupenda mtoto na kutoa matunzo bora kwa ajili ya mwanangu,”.

Muigiaji huyo aliyejizolea umaarufu katika uigizaji kupitia kundi la Kaole miaka ya 2000 amesema kuwa bado ana Imani ipo siku atapata mtoto kwani hakuna anayejua mipango ya Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *