Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rich Mavoko amekanusha vikali tetesi za kutoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Lulu Diva.
Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja kufuatia tetesi katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wanamahusiano ya kimapenzi jambo ambalo Rich Mavoko amelipinga vikali.
Mavoko amesema kuwa Lulu Diva ni rafiki wake sana lakini si wamahusiano kama inavyosambazwa katika mitandao ya kijamii kwani hakuna ukweli wowote kwakuwa yeye anamtu wake.
Wiki iliyopita Lulu Diva nae alipinga kutoka kimapenzi na Rich Mavoko akisema kuwa ni rafiki yake wa karibu na hana mahusiano nae.
Kwa upande mwingine Rich Mavoko amewataka mashabki wake wakae mkao wa kula kwani anatarajia kuachia nyimbo mpya hivi karibuni.