Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko amesema kuonekana karibu na lebo ya Kings Music Records ni kitu cha kawaida kwa sababu ni familia yake na ana ukaribu na Alikiba.

Kauli ya Mavoko imekuja baada ya watu kuhoji ukaribu wake na kiongozi wa lebo hiyo Alikiba kama anaweza kujiunga na lebo hiyo.

Rich Mavoko ameongeza kusema watashirikiana kwenye masuala ya kazi lakini kuhusu kusainiwa Kings Music Records ni suala ambalo hata hawaliwazii.

Mwanamuziki huyo kwasasa anafanya vizuri na albam yake mpya ambayo mapema mwezi huu alifanya sherehe ya kusikiliza albam yake hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *