Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama ameonekana na jeneza kwenye taarifa mpya juu kinachofuata kutoka kwenye EP yake iitwayo ‘CINEMA’.
Maua alitoa taarifa ya muendelezo wa Cinema iliyotokana rasmi Mei 20 2022 huku akionekana kuwa katika vazi jeusi lilioacha maswali ya kipi kinafuata.
Ikumbukwa katika hafla ya usikilizwaji wa EP hiyo, Maua alieleza kuwa itafuata filamu fupi itakayo angazia sehemu ya maisha yake ya ndani na nje ya muziki.
Hata hivyo haijabainika kama ni filamu ataachia hapo kesho Juni 08 2022 au ni video ya muziki kutoka kwenye orodha ya nyimbo zinazopatikana kwenye EP hiyo ya nyimbo saba(7).