Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amefunguka na kusema kuwa aliwahi kupitia wakati mgumu kiasi cha kutaka kuacha muziki.

Maua amesema kuwa muziki una changamoto sana na kwa upande wake alipitia vitu vingi kiasi alitaka arudi akaajiriwe tu.

Amesema “Muziki una changamoto, aisee nilipitia wakati mgumu na Bosi Ruge akanishauri nirudi kuajiriwa tu, pengine si mpango wa Mungu kuwa mwanamuziki.

Pia amesema kuwa Niliumia kwa kipindi hicho, ila sikukata tamaa, nikaendelea mbele kwa sababu nilikuwa napenda sana kuimba na ndiyo kitu kilicho ndani ya moyo wangu,’’.

Mwanamuziki huyo kwasasa ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *