Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amejibu malalamiko ya mashabiki baada ya kuachia wimbo wake mwingine mpya uitwao Baba Jeni.
Taarifa kwa umma chini ya ‘Sama Music’, Maua Sama adai kupokea malalamiko ya kwanini ameachia wimbo ‘Baba Jeni wakati ambao ‘ZAI’ bado unafanya vizuri.
Pia Maua Sama baada ya kuachia ‘Baba Jeni’ leo Nov. 20 aliongeza kuwa staili yake hiyo ya kuachia nyimbo kwa mfuatano ameipa jina la ‘UZAZI WA MPANGO’.
Mwanamuziki huyo ni mingoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri katika soko la muziki nchini Tanzania ambapo wanafanya vizuri sana.