Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amefunguka na kusema kuwa mwaka huu anatarajia kufunga ndoa.
Maua Sama amesema kuwa mwaka mungu akijalia mwaka huu ataolewa kama mambo yake yakienda sawa.
Awali zilienea tetesi kuwa, staa huyo anayebamba na Ngoma ya Nakuelewa amechumbiwa na mpenzi wake ambaye ni Mzungu lakini mwenyewe ameibuka na kukanusha.
Amesema kuwa “Nilishangaa kwa kweli hilo suala la kuchumbiwa na Mzungu kwani halikuwa la kweli, kuhusu kuolewa nimekuwa nikisikia kwa mashabiki sana, ndoa ni mipango, maombi yao yanaweza kunifanya nikatimiza hilo na inawezekana hata mwaka usiishe,”.