Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amethibitisha kuachana na mpenzi wake aliyekuwa akisemekana ni Mzungu ambapo amaedai Sababu ni Umbali wa wawili hao.

Mwanamuziki amesema kuwa umbali alipo mchumba wake kuna lockdown iliyopelekea wakaambiana ukweli kuwa uhusiano uishe na kwa sasa ni marafiki tu.

Maua amefunguka hayo wakati aliposaini dili la Ubalozi wa moja ya Club yenye eneo la michezo na kupumzikia,Ubalozi ambao atakuwa nao kwa Muda mrefu.

Pia Maua amesema hapendezwi na watu wanavyomshindanisha na msanii mwenzake Nandy, hii ikiwa ni baada ya kuachia wimbo wake wa Chuchumaa akidaiwa kutaka kushindana na Nandy aliyetoa wimbo wa ‘leo leo’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *