Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama hajapandishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa na wadau wengi wa muziki hapa nchini.

Maua Sama Wawili hao kwa pamoja alikamatwa na jeshi la polisi wiki iliyopita kwa tuhuma za kuidhalilisha nembo ya Taifa baada ya kupost video moja mtandaoni inayowaonyesha watu wakichezea hela za Tanzania.

Maua Sama hakuletwa mahakamani kama watu walivyotarajia huku wadau wa mambo wakidai kesi yake nitaanza kusikilizwa katikati ya wiki hii.

Mmoja kati ya mawakili ambao walijitokeza mahakamani hapo walidai wamewasiliana na jeshi la polisi na huwenda mrembo huyo akafikishwa mahakamani katikati ya wiki hii.

Soudy Brown amesomewa shtaka moja la kuweka maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali lakini dhamana ya kosa hilo iko wazi lakini anadaiwa bado anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuwa ana kesi nyingine ya kujibu.

Watuhumiwa wengine wameachiwa kwa dhamana baada ya kusomewa mashtaka ya kutumia blogs na YouTube bila kuwa na kibali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *