Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Matonya amefunguka na kukanusha taarifa za kujihusisha na uuzaji na usambazaji wa madawa ya kulevya.
Miaka kadhaa iliyopita zilisambaa taarifa kuwa mwanamuziki huyo amekamatwa na madawa ya kulevya nchini China na alitarajiwa kunyongwa.
Matonya amesema kuwa taarifa hizo zilimstua sana yeye pamoja na familia yake kutokana na sheria za kukutwa na madawa ya kulevya nchini China ambapo adhabu yake inakuwa ni kunyongwa au kufungwa maisha jela.
Pia Matonya amesema kuwa sababu ya kuzushiwa skendo hiyo ni kutokana na maisha yake aliyokuwa anaishi wakati alikuwa afanyi show yoyote ndani nan je ya nchi.
Kwa upande mwingine Matonya amefunguka kuhusu taarifa za yeye kuwa na bifu na Ali Kiba ambazo amedai ni stori tu ambazo watu wamekaa wametunga kwani yeye hana bifu na msanii yoyote nchini.