Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Matonya amedai kuwa hakujua kama amevalishwa vazi la kike ‘Baibui’ katika video yake mpya ya ‘Kiherehere’.
Matonya amesema kuwa yeye hakujua kama lile vazi ni la kike kwasababu amepewa na director aliyeongoza video hiyo aliyoiachia hivi karibuni.
Matonya amefafanua hilo baada ya watu wengi kuanza kumfikilia ndivyo sivyo kutokana na kuonekana kuvaa vazi hilo angali yeye ni mtoto wa kiume.
Pia Matonya amesema kuwa anapenda video zake ziwe za tofauti na watu wengine wanavyofanya ili ziwe bora sana na mashabiki zake wafarijiki na muziki wake.
Kwasasa mwanamuziki huyo anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Kiherehere aliouchia hivi karibuni na unaendelea kufanya vizuri.