Wafanyakazi wa kike wa nyumbanni kutoka nchin Tanzania walio nchini Oman na sehemu nyingine za nchi za kiarabu UAE, wanadhulumiwa kimwili na kingono.
Hayo yamethibitishwa na shirika la kitetea haki za binadamu, Human Rights Watch (HRW) baada ya kufanya utafiti.
Kwenye ripoti iliyotelewa leo, HRW ilisema kuwa kuna maelfu ya wafanyakazi wa nyumbani kutoka Tanzania wako nchini Oman na UAE.
Watafiti wake waliwahoji 50 kati yao na kugundua kuwa karibu wote walipokonywa pasipoti zao walipowasili na kulazimiswa kufanya kazi hadi masaa 21 kwa siku bila kupumzika.
Wafanyakazi waliotoroka waajiri dhalimu na maajenti walisema kuwa polisi au balozi zao ziliwalazimisha kurudi la sivyo wangekosa mishahara yao hali iliyowachukua muda mrefu kutafuta pesa za kuwawezesha kurudi nyumbani.
Walisema kuwa walilipwa pesa kidogo kuliko zile waliahidiwa, au walikosa kulipwa kabisa, wakalazimishwa kula chakula kulichooza au mabaki ya chakula na kutukanwa kila siku, na pia kudhulumiwa kingono.