Video vixen maarufu Bongo, Agnes Gerlad ‘Masogange’ amefunguka kusema kuwa mwaka 2017 ulikuwa mwaka mbaya kwake kutokana na misukosuko aliyokutana nayo ndani ya mwaka huo.
Masogange amedai kuwa anauchukia sana mwaka 2017 kutokana na mambo magumu yaliyompata akiri kuusubiri kwa hamu mwaka 2018.
Video vixen huyo amekiri kuwa mwaka huu ulikuwa mgumu sana kwake hadi kupelekea kuuchukia.
Mapema mwaka huu Masogange alikamatwa na kifikishwa kituo cha polisi baada ya kituhumiwa kwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya ambapo hadi sasa kesi yake inaendelea.
Ingawa baada ya tuhuma hizo na kukaa rumande kwa siku chache na uchunguzi kufanyika wengi wao waliachiwa huru lakini Masogange alikuwa mmoja wa watuhumiwa waliofunguliwa mashtaka mahakamani na hivyo kupelekea Agnes kuwa na kipindi kigumu.
Masogange amekiri kuwa tuhuma hizo zimemfanya mambo yake yamesimama pia amedai biashara zake nyingi zimesimama kwa mwaka huu kutokana na kukosa muda wa kwenda kufatilia kutokana na kuhitajika mahakamani mara kwa mara.