Video queen wa Bongo, Agnes Masogange amekatwa na Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam akituhumiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Masogange anashikiliwa na Jeshi hilo katika Kituo Kikuu cha polisi (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Video queen huyo amekamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba, mpaka muda huu bado anashikiliwa kituo cha polisi kutokana na tuhuma hizo zinazomkabili.
Masogange anaungana na wasanii wengine walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya katika jiji la Dar es Salaam.
Vita ya madawa kupambana na dawa za kulevya zimeanzishwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo ameungwa mkono Serikali kuu kuhusu suala hilo.