Naibu waziri wa mambo ya ndani, Hamad Masauni amelitaka jeshi la polisi na wasimamizi wa sheria kutofumbia macho wanaovunja sheria za barabara nchini ili kupunguza ajali.
Naibu waziri, Masauni amesema kama wananchi wakiamua kufuata sheria zilizowekwa ajali zitapungua.
Masauni amesema “Jeshi la polisi na wasimamizi wengine wa sheria, endeleeni kuchukua hatua kali na madhubuti za kukabiliana na hali hii bila kumuogopa wala kumuonea aibu mtu yeyote”.
Aliongeza kwa kusema kuwa “Makundi yote ya utumiaji wa barabara yana wajibu mkubwa ya kuzitumia barabara zetu, tutambue wote tuwajibike kupambana na zile ajali za barabarani, hivyo inatubidi tushirikiane, kuelekezana na kumuonya kila mmoja wetu anapovunja sheria na kanuni za usalama barabarani,”.
Kwa upande Masauni amelitaka shirika la viwango nchini Tanzania (TBS) kuhakikisha magari na matairi yote ya nchini ili kupata bidhaa zenye ubora zitakaosaidia kupunguza ajali za mara kwa mara.