Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga marufuku wanasiasa kutumia nyumba za ibaada kufanya kwa shughuli za kisiasa visiwani humo.
Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar, Mh. Mohammed Aboud amesema kuwa viongozi wa dini na kamati zao katika nyumba za ibada watakaoruhusu wanasiasa kuendesha shughuli hizo, watawajibika kwa mujibu wa sheria za nchi.
Waziri huyo amesema “Ninatoa hoja ya kuzungumza nanyi kupitia taarifa hii kwa lengo la kuelimisha na kuwatahadharisha kwa mwenendo wa baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia nyumba za ibada hususani misikiti, kuwa ni majukwaa ya kisiasa kwani jambo hilo ni hatari sana kwa mustakabali wa Zanzibar, Tanzania na wananchi kwa ujumla,”.
Hatua hiyo inakuja baada ya baadhi ya viongozi kutumia nyumba za ibada kwa ajili ya kufanya mikutano ambapo kwasasa ni kosa kufanya hivyo.