Kocha wa Ubelgiji, Roberto Martinez amemteua mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Barcelona na timu ya taifa ya France, Thierry Henry kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

Mara baada ya uteuzi huo Martinez amesema kwamba Thierry ni mtu mzoefu sana kwenye masuala ya soka la kimataifa ndiyo mana ameamua kuwa msaidizi wake kwenye timu hiyo ya Ubelgiji.

Kwa upande wake Henry amesema anashukuru na anajisikia furaha sana kuteuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo ya taiafa ya Ubelgiji.

Henry pia aliwahi kuwa kocha wa timu ya vijana ya Arsenal ambapo aliacha kazi hiyo baada ya kupata kibarua kwenye kituo cha runinga cha Sky Sports.

Martinez tayari ameita kikosi chake kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Uhispania Sepetemba 1 mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *