Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka na kusema kuwa ana Imani kuwa siku moja atafanya shoo katika ukumbi wa O2 Arena uliopo London nchini Uingereza.

Marioo amesema hayo baada ya kufanya Tukio kubwa la Kihistoria pale Mlimani City Januari 28,2023 ambapo alizindua albam yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘The Kid You Know’.

Marioo ameweka Imani yake wazi kuwa Anaamini ndani ya Mwaka Huu atatumbuiza katika Ukumbi mkubwa wa kiburudani wa 02 ARENA unaopatikana London huku akisema kuwa anaamini Staa wa Muziki kutoka Nchini Nigeria Davido atamsaidia kwenye hilo.

Licha ya Kolabo ya Marioo na Davido Kufeli kutokana na wote wawili kukosa nafasi bado inaonekana kuna ukaribu wawili hao bado wanao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *