Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka na kusema kuwa kwanini kwa upande wa Tanzania kumekuwa na uhache Ssna wa wasanii kuliwakilisha Taifa Kimataifa Katika Matamasha Makubwa Duniani.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya Diamond Platnumz kuwa msanii pekee kutoka Tanzania kufanya show ya kimataifa nchini Ureno.

Marioo amesema kuwa “Kuna Mtu Aliwahi Kuniambia Kitu Nikafikiria Nikaona Ni Kweli,,Ujue Tofauti Ya Sisi Na Wenzetu Mfano Kama Wanigeria Wanaishi Sehemu Mbalimba Nje Ya Nchi Yao Na Wanahit Atleast Na Sisi Wasanii Wengine Wangekua Wanahit Huko Huko Mwanza Au Sehemu Zingine Sasa Huku Kila Mtu Anakuja DAR Tunajikuta Wote Tupo Hapa Kwahiyo Inafika Muda Unawaza Kwamba Kama Nikimpa Shavu Huyu Itakuwaje Wote Tukikutana Kidimbwi.”

Pia amesema kuwa “Lakini Pia Wenzetu Ni Wanyamwezi Yani Wana Uchungu Na Taifa Lakini Sisi Hapa Kila Mmoja Anajiangaia Mwenyewe Kwamba Mimi Na Ugali Wangu Tu Anavyojipambania Yeye Anaona Kama Analipambania Taifa.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa Ni Kweli Iko Hivyo Lakini Kuna Namna Ya Kulipambania Taifa Kwenye Upande Wa Kusapoti Watu Wengine Kingine Pia Brothers (Wasanii Wakubwa) Wanahofia Madogo Hawaeleweki Ndio Maana Wenzetu Wanakua Wanatuzidi”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *