Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amesema kuwa ngoma ya yake ya Mama Amina imempa nguvu kubwa kwenye mziki yake kwa sababu alifanya kwa gharama kubwa na ilifanya vizuri.

Kauli mwanamuziki imekuja kufuatia mbunge wa Morogoro vijijini na meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale kusema kuwa wimbo wa Marioo uitwao Mama Amina ulipaswa kufungiwa kutokana na kuimba matusi.

“Hii ni moja kati ya project iliyonipa nguvu na moyo wa kutokuogopa na kuwekeza kwenye Mziki wangu kwa ajili ya Taifa maana hizi collabo na hii video nilifanya kwa gharama kubwa sana na goma likaja likalipuka” ameandika Marioo 

Marioo amesema kuwa ameshangazwa sana na kauli ya meneja huyo kwani ahukuzi muziki bali inadidimiza muziki wa Bongo Fleva nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *