Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo ameunga mkono harakati za mchekeshaji Eric Omondi ambaye hivi karibuni amekuwa akidai mabadiliko kwenye soko la muziki nchini Kenya.
Kupitia Instastory yake Marioo amesema kuwa kuna tabia ya baadhi ya wadau wa muziki hata hapa Tanzania wamekuwa wakiwapa thamani kubwa wasanii wa nje kuliko wasanii wa ndani.
Marioo ameandika “Unakuta anakuja msanii kutoka Nigeria au Afrika Kusini anawimbo wake mmoja ila wanavyomjali kama wanataka kufunga nae ndoa”.
Nyongo ya Marioo inazidi kupasuka ” Wasanii wao wanatuchukulia poa. Hii kitu inaboa sana, yani sisi huku bongo wageni wanapewa 90% sisi 10% hii kitu imekaa kimiyeyusho sana”.