Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka na kusema kuwa Tanzania kumekua na Tabia ya wasanii kuwekeana Kinyongo kwa msanii mmojawapo anapotengeneza Hit Kubwa kuliko wasanii wengine.

Marioo amesema kuwa unakuta Ngoma yako ndio namba 1 kwa wakati huo. lakini badala ya wasanii wote kuishikilia mfike mbali, wao ndio wanakua namba 1 kuikandamiza na kuweka vikwazo ili ifeli hiyo ngoma”

Angalia wenzetu Nigeria, Ile Buga imetoka Video Jana Mastaa wakubwa wote wameipa Support yani Taifa linaongelea Ngoma Moja tu, na wanahakikisha inavunja rekodi hata ya ngoma zao.

“Kuna Kipindi Kimefika, inabidi tukubali kuwa Sisi ndio wasanii wakubwa wa Muda huu na hivi vitu huwa vinaenda na muda hata kwa mataifa mengine yaliyoendelea”

Pia amesema kuwa “Ukiangalia Wenzetu Nigeria, Wasanii wakubwa walikuwepo kina D Banj, 2 Face, Don Jazzy wakina P Square, Baadae kikaja kizazi cha Kina Davido, Wizkid au Burna Boy, lakini sasa hivi unaona wamekuja madogo wamoto sana na wamepewa Ukubwa kwamba wao ndio wakubwa kwa sasa – wapo kina Rema, Joeboy, Fireboy, Omah Lay au Kizz Daniel”

Amemaliza kwa kusema kuwa “Lazima tukubali kuwa kuna muda wasanii hawa wameshapita muda wake na sasa tupo kwenye kizazi fulani, Wasanii wa Tanzania Wakubwa Miaka yote ni Wale Wale”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *