Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka na kusema kuwa ofa za kujiunga na lebo ya Kings Music Records na Wasafi hazikufanikiwa kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.

Marioo amefunguka hayo baada ya kuulizwa kama yupo tayari kujiunga na lebo hizo kubwa za muziki hapa nchini amba zinamilikiwa na Alikiba na Diamond Platnumz.

Mkali huyo wa Mama Amina ameendelea kusema kuwa kutokana na uwezo wake wa muziki kwasasa hawezi kuwa chini ya lebo hizo kwani anafanya vizuri.

Amesema kuwa “Ukizungumzia Kings Music na Wasafi ni lebo kubwa sana East Africa na Africa kwa ujumla, lakini hizo ofa hazijawahi kutokea na hata kama zimetokea hazikufanikiwa kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu”.

Pia Marioo amesema sasa hivi hana mpango wa kusainiwa lebo yoyote hapa Africa ila anapenda jinsi Kings, Wasafi na Konde Gang wanavyofanya kazi kwa wasanii wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *