Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amesema kuwa kwa wasanii wa kizazi chake hakuna wa kushindanishwa naye kwa kuangalia vigezo vya ngoma kali na uandishi kwa ujumla.

 Marioo amesema hataki kuwaweka wasanii waliomtangulia kwa sababu atakuwa anajilinganisha nao ila kwa kizazi chake haoni wa kumfikia.

“Nikiangalia kwenye ‘generation’ yangu sioni wa kumuweka kwa kuangalia hits zake na zangu toka nianze mimi nafumua tu, japokuwa nao wanafanya vizuri, wanasizi na wanaibuka tena”.

Mwanamuziki huyo kwasasa anaendelea kufanya vizuri kutokana na ubora wa nyimbo zake kuwabamba mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *