Nchi ya Marekani imendeleza vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwemo marufuku kwa biashara ya mafuta na kutwaliwa kwa mali ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Azimio lililowasilishwa kwa wanachama wa baraza la ulinzi wa Umoja wa Mataifa, linakuja baada ya jaribio la sita la nyuklia kufanywa na Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini inadai kuunda bomu la haidrojeni na imekwua ikitishia kuishambulia Marekani.

Korea Kaskazini tayari iko chini cha vikwazo vya kuitenga vilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa, ambavyo vina nia ya kuulazimisha utawala wa nchi hiyo kusitisha mipango yake ya nyuklia.

Mwezi Agosti vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa vilipiga marufuku kuuzwa kwa mkaa wa mawe kutoka Korea Kaskazini ya thamani ya dola bilioni 1.

Pendekezo hilo la Umoja wa Mataifa linataka kuwekwa marufuku kabisa ya kuuzwa kwa bidhaa za mafuta kwenda Korea Kaskazini.

Pia pendekezo hilo linataka kutwaliwa kwa mali ya Bwa Kim na serikali ya Korea Kaskazini na pia kimpiga marufuku Kim mwenyewe na maafisa wengine wa vyeo vya juu kusafiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *