Marekani imeiwekea vikwazo nchini ya Iran kufuati hatua yake ya hivi majuzi ya kulifanyia jaribio kombora.

Wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza hatua dhidi ya watu 13 na kwa kampuni kadha leo Ijumaa.

Rais Donald Trump aliandika mapema kwenye mtandao wa twitter kuwa,”Iran inacheza na moto, hawana shukran jinsi Obama alikuwa mkarinu kwao, Si mimi!”

Lakini Iran imesema kuwa hauwezi kulegeza kamba kutokana na vitisho visivyo na maana vya Marekani, kutoka kwa mtu asiye na juzi.

Kati ya makudi yaliyowekewa vikwazo yako nchi ya miliki za kiarabu , Lebanon na China.

Wiki hii mshauri wa masuala ya ulinzi Michael Flynn, alisema kuwa Marekani inaionya Iran kufuatia jaribio hilo la kombora.

Lakini waziri wa mashauri ya nchi za kigeni kwa Iran Mohammad Javad Zarif, leo Ijumaa aliandika kwenyr mtandao wa twitter akisema kuwa Jamhuri hiyo ya kiislamu haitikizwi na vitisho vya Marekani.

Amesema kuwa Iran haina mapango yoyote ya kutumia jeshi lake dhidi ya nchi yoyote bali kujilinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *